Ufikapo wakati ambapo mtu huzama
Maisha hukulemea
Kilio ndicho chako kila wakati
Alfajiri na jioni wamsaka Mola
Akuinue,
Angalau akukumbuke
Maadui wamekuzingira
Hakuna cha kukuridhisha, cha kukutuliza roho
Kama Ayubu alipoteseka duniani na alimcha Mungu wakati wote
Hatujajaribiwa mpaka tukapatana na kifo
Nitamkimbilia Bwana
Yeye ndiye penzi langu
Maadui wanaposherehekea vita vyangu
Sitamsuta Maulana
Nanyenyekea mbele zake
Nikosapo nguvu
Niangukapo
Nilemewapo
Nikishushwa moyo na dunia
Napata matumaini Calvary
Alisulubiwa juu yangu
Alinifia
Akafufuka
Ili nami nipate uhai na uhai halisi
siwezi simama kwa upweke
Yesu ananishikilia kila wakati
Ata wakati huu ambapo ndugu yangu anaugua
Yesu ni Bwana
Wakati marafiki hawapatikani
Yesu yupo
Pesa haipo
Yesu yupo
Usaliti wa wapenzi
Yesu yupo
Nipo,ju Yesu yu hai ndani yangu
Siwezi simama wima pekee yangu
Lakini, nasimama juu yake Yesu!!!!
No comments:
Post a Comment
Share this, put a smile on someone's face :-)